Katekesi Kwa Familia na Vijana

picha watoto wetuwatoto wetu

MAADHIMISHO YA MIAKA

18 YA RADIO MARIA TANZANIA

MWAKA 2014 YANATARAJIWA KUADHIMISHWA

KATIKA JIJINI LA ARUSHA

 UNAKARIBISHWA KATIKA MICHANGO YA HARI NA MALI

KARIBU RADIO MARIA TANZANIA

Rate this Content 1 Votes

MIKOCHENI DAR ES SALAAM

 

Masafa ya RMTz RADIO MARIA kwa sasa inapatikana dunia nzima kupitia mtandao yaani online kupitia www.radiomariatz.co.tz

au www.tunein.com/radio maria

TUMSAIDIE MAMA YETU BIKIRA MARIA KATIKA UINJILISHAJI, NAE APATE KUTUSAIDIA

 

 

RADIO MARIA 2014, uwe nyumbani, ofisini shuleni na mahala popote ulipo , FANYA UTUME WAKO TIMIZA MALENGO YAKOSmilena radio maria sauti ya kkristo nyumbani mwako

                               TAARIFA YA HABARI

 

Mapadre wametakiwa kuungana na YESU KRISTO ili waweze kuleta Msamaha na Usuluhishi kwa ulimwengu mzima.

Hayo yamesemwa leo Mjini SONGEA na Askofu Mstaafu EMANUEL MAPUDA wa Jimbo Katoliki la MBINGA wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya kubariki MAFUTA iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Kuu la SONGEA.

Askofu MAPUNDA amesema  kuwa, wanapobariki  MAFUTA Matakatifu  ambayo yatatumika  kwa Wagonjwa, Daraja takatifu na katika Sakramenti nyingine, YESU anawashirikisha waliopewa daraja takatifu katika kuungana naye ili kuweza kuleta msamaha na usuluhishi wa kweli.

Amesema YESU anawafikisha kwenye kilele cha Ukombozi na anawaalika waungane nae ili waweze kushiriki msamaha wa dhambi.

Wakati huo huo  Askofu MAPUNDA amewataka Waamini kujongea na kuungana na YESU aliyepakwa MAFUTA Matakatifu na anayeleta usuluhisho kamili na wa kweli ili tupate upya wa maisha na msamaha kamili wa dhambi zetu. 

Shirika la Maji Safi na Maji Taka DAR ES SALAAM (DAWASCO) limewaomba wakazi wa Jiji la DAR ES SALAAM kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha mpito kutokana na mvua kubwa zilizo sababisha uaharibifu wa miundo mbinu ya Maji katika maeneo tofauti hali iliyo pelekea kukosekana kwa huduma ya maji.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano wa DAWASCO Bi EVA LYARO wakati wa ziara ya kukagua miundo mbinu ya Maji iliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha maeneo mbali mbali hapa nchini.

Ameeleza kuwa Mitambo ya Maji ya RUVU CHINI na Mitambo ya MTONI Wilaya ya TEMEKE imezimwa kutokana na Maji ya mvua kuharibu Bomba la kupoozea Maji sanjari na Mashine za Maji kufunikwa na maji mengi hivyo wakaamua kuzima hadi hali itakapo tengemaa.

Hata hivyo DAWASCO ameeleza kwamba kukatika kwa Bomba la Maji la JANGWANI imesababisha Hospitali ya MUHIMBILI kukosa Maji sanjari na maeno ya katikati ya jiji hivyo wanaomba radhi kwa usumbufu wote ulio jitokeza ila mafundi wapo katika matengenezo ili kuhakikisha huduma ya maji inarejea.

Wanawake hapa nchini wameshauriwa kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango kwa kuwa zinasababisha KANSA kwa akina mama waliowengi na badala yake watumie njia ya uzazi wa asili kadili ya mpango wa MWENYEZI MUNGU.

Ushauri huo umetolewa na Naibu wa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la SONGEA Padre CAMILIUS HAULE wakati wa Ibada ya Misa ya Jumapili ya MATAWI iliyofanyika katika Kanisa Kuu la KIASKOFU mjini SONGEA.

Padre HAULE amesema dawa za uzazi wa mpango kwa akinamama zina madhara makubwa ambayo hupelekea kifo kwa akinamama wanaotumia dawa hizo hivyo ni vyema kuacha kutumia dawa hizo ili kunusuru maisha yao na ya watoto wanao wazaa.

Aidha amewataka akinamama kutumia njia ya uzazi wa asili kadili ya mpango wa MWENYEZI MUNGU ambayo ni salama na haina madhara yoyote kwa akinamama na kuongeza kuwa kutumia dawa za uzazi wa mpango ni kwenda kinyume na matakwa ya MUNGU ni kujiua wenyewe.

Hata hivyo Padri HAULE amefafanua kuwa imefika wakati sasa kwa akinamama kuacha kuendelea kudanganywa kuwa dawa hizo hazina madhara, huku akisisitiza kuwa Kanisa Katoliki halitaacha kufundisha ukweli kuwa dawa za uzazi wa mpango ni uuaji wa siri kwani dawa hizo husababisha maumivu makali, na magonjwa kama KANSA na hatimaye vifo.

Wazee wanaoishi katika Kambi ya Wazee ya NJORO Mkoani KILIMANJARO wameiomba Serikali na Mashirika binafsi kuwasaidia Maabara katika kliniki iliyopo ndani ya Kambi hiyo pamoja na gari kwa ajili ya kuwasaidia Wazee wanaoandikiwa rufaa kwa ajili ya kwenda Hospitali.

Wazee hao wametoa ombi hilo muda mfupi baada ya kupokea
msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa uongozi na wanachama wa chama cha waigizaji na wacheza Filamu Mkoani KILIMANJARO (KDFAA).

Wameleza kuwa kutokana na kuwapo kwa Kliniki,wamekuwa wakikosa
nauli ya kwenda Hospitali pindi wanapotakiwa kwenda katika Hospitali
za rufaa ikiwemo Hospitali ya KCMC na MAWENZI jambo ambalo linawafanya kuishi kama wametelekezwa.

Kwa upande wake Katibu wa chama hicho Bwana DITRAM NGONYANI kwa niaba ya viongozi wenzake amesema lengo la ziara yao ni kuzungumza
na wazee hao ikiwa ni pamoja na kufahamu changamoto wanazo kabiliana
nazo katika maisha yao.

Hata hivyo ameiomba Serikali pamoja na wadau mbali mbali kujitokeza katika kuwa saidia kuwajengea uzio Wazee hao kwani wapo hatarini kutokana na imani za kishirikina.

Bohari ya Dawa (MSD) kwa kushirikiana na Wahisani katika kuboresha huduma ya Afya inaendelea na Mpango wa kupanua MAGHALA ili kuongeza nafasi za kuhifadhi dawa na vifaa tiba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini DAR ES SALAAM Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Bwana EDWAD TERRY amesema kuwa tayari MAGHALA ya Kisasa yaliyokamilika yameanza shughuli ya kuhifadhi Dawa na Vifaa Tiba

Ameeleza kuwa lengo kubwa la MSD kuwa na MAGHALA mengi ni kuboresha upatikanaji wa Dawa na Vifaa tiba pamoja na huduma ya Afya kwa uharaka na kwa wakati unaostaili kwa Wananchi.

Aidha Bwana TERRY ameongeza kuwa ununuzi wa Dawa na Vifaa Tiba unazingatia miongozo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo Dawa na Vifaa vyote lazima visajiliwe na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati Vitendanishi vya Mahabara husajiliwa na kuidhinishwa na Bodi ya Maabara Binafsi (PHLB) kabla ya kuagizwa na kusambazwa katika Hospitali zote pamoja na vituo vya Afya.

Hata hivyo amesisitiza kuwa MSD itahakikisha wananchi wanapata  huduma za Afya nchini kote kwa wakati.

Jeshi la polisi kikosi cha Reli nchini limewatunuku vyeti na Zawadi mbali mbali Askari wake TISA ambao walifanikiwa kukamata mali mbali mbali za wizi sanjari na waalifu watatu mwaka jana katika mazingira tofauti ya  Mkoa wa DAR ES SALAAM na PWANI.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutunuku zawadi hizo Kamanda wa Kikosi cha Reli TANZANIA SACP SAADA JUMA HAJI amesema Askari hao waliweza kukamata na kuokoa mali hizo za wizi ikiwemo silaha, nondo na mataluma ya Reli.

Aidha kamanda SAADA amesema jeshi hilo limeamua kufanya hivyo kutokana na utiifu na nidhamu, hivyo ametoa wito kwa Askari wengine wa kikosi cha Reli nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha kutengeneza mianya ya rushwa katika kazi zao ili waweze kujijengea heshima katika jeshi hilo.

Wakizungumza kwa niaba ya Askari wenzao waliopewa vyeti hivyo Kopro wa Upelelezi Kikosi cha Reli DAR ES SALAAM D/CPL BERNAD MINJA na D/CPL Kopro DISMASI wamesema kwa upande wao walifanikiwa kukamata Reli 48 na Silaha aina ya Shotgani katika eneo la KODOMORE Mkoani PWANI.

Baba Mtakatifu FRANSISKO anatarajia kutoa zawadi ya vitabu vidogo vya Injili, vipatavyo elfu moja mia mbili, kama zawadi ya PASAKA kwa Wafungwa katika Gereza Kuu la Malkia wa Mbingu la mjini ROMA.

Zawadi ya Baba Mtakatifu itawasilishwa kesho, na Askofu Mkuu KONRAD KRAJEWISKI wakati atakapo tembelea Gereza hilo.

Kitabu hicho kidogo cha Injili chenye kuwa pia waraka wa Matendo ya Mitume, Jumapili iliyopita pia kiligawiwa kwa Waamini waliofika kumsikiliza Baba Mtakatifu wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu PETRO.

Baba mtakatifu FRANSISKO pia aligawa kitabu hizo kamazawadi ya pasaka kwa waamini waliohudhuria Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu GEORGE Mkuu la MAGLIANA la Mjini ROMA.

Polisi nchini NIGERIA wamesema, shule moja ya wasichana imeshambuliwa katika Jimbo la BORNO Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo huku zaidi wasichana mia mbili wakihofiwa kutekwa nyara na washambuliaji hao.

Habari zinasema kuwa washambuliaji hao wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la wapiganaji la BOKO HARAM.

Aidha Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili wameuawa huku mali ikiharibiwa vibaya wakati wa shamblizi hilo lililo tokea Mjini CHIBOK.

Hapo jana, zaidi ya watu SABINI, wameuawa katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini ABUJA ambapo Kundi la BOKO HARAM pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.

 

 

 

 

 

Changia

Senti tano kama ya mjane ni mchango muhimu kwa Radio Maria! Kwa ukarimu wako... Kristo atafika katika familia nyingi!

Tutumie mchango na ahadi yako Radio Maria Tanzania,

Plot 125,
Mikocheni Industrial Area,
P.O.Box 34573,
Dar Es Salaam,
Tanzania.

Facebook

Rate this Content 1 Votes

           kuwa nasi kupitia  hapa

 

 

Modified 14/04/2014